Kamishna wa uhamiaji mkoa wa Kilimanjaro Johanes Msumule akizungumza na wanahabari ofisini kwake baada ya kukamatwa kwa wahamiaji haramu 11 wilayani Rombo
Afisa wa uhamiaji wilaya ya Rombo akiwasindikiza watu wawili ambao wanatuhumiwa kuwa ndio wahusika wa usafirishaji wa wahamiaji haramu hao.
Bi. Leokadia Tarimo raia wa Tanzania na Bw. Paulo Endevayesu raia wa Burundi ambao wanatuhumiwa kujihusisha na biashara ya kusafirisha wahamiaji haramu hao
Wahamiaji haramu waliokamatwa wilayani Rombo katika moja ya nyumba ya wageni.
Askari wakiwa katika gari lililopeba wahamiaji haramu hao waliokamatwa wilayani Rombo katika moja ya nyumba ya wageni.
Na Dixon Busagaga , Moshi.
WIMBI
la wahamiaji haramu kuingia nchini limeendelea kushika kasi katika siku
za karibuni kufuatia kukamatwa kwa wahamiaji haramu wengine 11 raia wa
Ethiopia katika kijiji cha Mlele kata ya Mashati wilayani Rombo wakiwa
wamehifadhiwa katika nyumba ya kulala wageni.
Tukio
la kukamatwa kwa wahamiaji hao linakuja ikiwa ni wiki moja imepita
baada ya kukamatwa kwa kundi jingine kubwa la wahamiaji haramu wapatao
56 katika kijiji cha Jiungeni wilayani Same wakiwa katika harakati za
kufanya safari kuelekea nchini Afrika Kusini kwa lengo la kutafuta
kazi.
Kamanda
wa polisi mkoa wa Kilimanjaro Robert Boaz amesema kuwa wahamiaji hao
walikamatwa juzi majira ya saa 7 mchana baada ya askari polisi waliokuwa
doria kupata taarifa ya kuwepo kwa wahamiaji hao haramu katika moja ya
nyumba za wageni.
“Jana(Juzi)
saa 7 mchana askari wakiwa doria walipata taarifa kuwa kuna wahamiaji
haramu na kwamba kwamba wamefichwa kwenye nyumba moja katika kijiji cha
mlele kata ya Mashati na askari baada ya kufika katika nyumba hiyo
waliwakuta”alisema Kamanda Boaz.
Alisema
baada ya kukamatwa kwa wahamiaji hao polisi ilianza ufuatiliaji juu ya
wahusika waliowaingiza nchini na kuwahifadhi ndipo wakafanikiwa
kumkamata mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina la Leocadia Gapiti
ambaye anadaiwa kuwa ndiye mmiliki wa nyumba hiyo.
“Tumemkamata
mwanamke mmoja anaitwa Leokadia Gapiti ambaye alikuwa amewahifadhi
kwenye nyumba hiyo na mwingine Paulo Endevayesu ambaye ndiye wakala
halisi ambaye alikuwa anawasafirisha watu hao.”alisema.
Kamanda
Boaz alisema uchunguzi zaidi unafanyika ili kujua watu hao walikuwa
wanatoka wapi wanaenda wapi na kwamba pindi utakapo kamilika
watafikishwa mbele ya vyombo vya sheria.
Kwa
upande wake kamishna msaidizi wa uhamiaji mkoa wa Kilimanjaro Bw.
Johanes Msumule alisema wamebaini kuwepo kwa mtandao mkubwa katika suala
hilo na kwamba tayari wanaendelea kuwahoji watu wawili waliokamatwa
ambao ni Leokadia na Paulo Endevayesu raia wa Burundi.
Alisema
katika kipindi cha wiki tatu kilichopita tayari wamesafirishwa zaidi ya
wahamiaji haramu 74 kurudi nchini mwao Ethiopia ambapo kundi la kwanza
lilikuwa la wahamiaji haramu 18 ambao walikabidhiwa kwa askari wa Kenya
.
Alisema
kundi la pili lilikuwa la wahamiaji haramu 56 lililokamatwa hivi
karibuni lilisafirshwa hivi karibuni kupitia mpaka wa Namanga hadi
katika kijiji cha Moyale kilichopo mpakani ma nchi za Kenya na
Ethiopia.
Tukio
la karibuni lilihusisha kukamatwa kwa wahabeshi 56 katika kijiji cha
Jiungeni –Same wakiwa katika Lori aina ya Fuso, yenye namba za usajili,
T188 AYU,linalotajwa kama mali ya kampuni ya ELyimo Trans ya Mjini Moshi
likiwa na jina la Godbless Mbasha wa mkoani Manyara.

No comments:
Post a Comment