Umati wa watu kutoka maeneo mbali mbali ya jiji la Dar,wakiwa wamefurika kwa wingi katika eneo la ufukwe wa Coco Beach kwa ajili ya kupunga upepo na kuendelea kuisherehekea sikukuu ya Krismas.Coco Beach ndio eneo pekee linaloweza kuwakutanisha watu mbali mbali hasa wale wa hali ya kawaida kama kina sie na kutufanya tuzisherehekee sikukuu mbali mbali kwa furaha zote.
Kijani kikiwa kimetawala kwenye Ufukwe wa Coco.
Hivi ndio mambo yalivyokuwa katika Ufukwe wa Coco leo.
Mdau akijiandaa kuwapigisha raidi ya majini madogo.
Watoto wakiogelea kwa raha zao.
Kuziba pua pia kumo ukiwa majini.
Hii ndio raha ya Beach,hata kama hujui kuogelea kama mie basi utachezea maji namna hii.











Jeshi la police lilitangaza watoto hawataruhusiwa kuingia kwenye maji na honi ni akina nani.au ndo zile ahadi zisizotekelezeka!!
ReplyDelete