Mohamed Achume anayelelewa katika kituo cha kule yatima cha New Life Orphans Home kilichopo Kigogo jijini Dar es Salaam akikabidhiwa msaada wa gunia la mchele na Afisa habari wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Ally Changwila (kushoto) ikiwa ni sehemu ya vyakula mbalimbali vilivyotolewa na mamlaka hiyo kwa ajiri ya watoto hao kusherehekea sikukuu ya krismasi.
Afisa
habari wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Ally Changwila
akiwakabidhi msaada wa madaftari Rahma Seif na Yusra Yahaya ambao ni
watoto wanaolelewa katika kituo cha yatima cha New Life Orphans Home
kilichopo Kigogo jijini Dar es Salaam. Vyakula mbalimbali vilitolewa
ikiwemo mchele na Maharage.
Afisa
habari wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Ally Changwila
akiwakabidhi msaada wa mafuta ya kula Mohamed Achume ambaye ni miongoni
mwa watoto wanaolelewa katika kituo cha yatima cha New Life Orphans Home
kilichopo Kigogo jijini Dar es Salaam. Vyakula mbalimbali vilitolewa
ikiwemo mchele na Maharage.
Afisa
habari wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Ally Changwila
(kushoto) akiwa na wafanyakazi wenza katika picha ya pamoja na baadhi ya
watoto yatima wanaolelewa katika kituo cha New Life Orphans Home
kilichopo Kigogo jijini Dar es Salaam. Baada ya kuwa kabidhi msaada wa
vyakula mbalimbali yakiwemo mafuta ya kupikia , mchele na sukari.

No comments:
Post a Comment