Saturday, July 28, 2012

Mechi ya Yanga na Azam uwanja wa Taifa hivi sasa......Yanga yaongoza kwa bao 1-0 na mchezo unaendelea

 Kikosi cha Yanga
 Kikosi cha Azam
 Mgeni rasmi katika Mchezo wa leo ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Mh. Said Meck Sadick.na hapa alikuwa akitambulishwa kwa wachezaji wa Timu ya Yanga.
 Mgeni Rasmi akisalimiana na wachezaji wa Azam.
 Picha ya Pamoja.
 Mlinzi wa timu ya Azam,Said Moradi akiwania mpira na Mshambuliaji wa Timu ya Yanga,Said Bahanuz wakati wa mchezo wa fainali ya Mashindano ya Cecafa Kagame cup unaoendelea hivi sasa uwanja wa Taifa jijini Dar.
 Mshambuliaji wa Yanga,Hamis Kiiza akiondoka na mpira huku mlinzi wa Azam,Jabir Aziz akimkimbiza kwa kutaka kumzuia mshambuliaji huyo.Kipindi cha kwana kimemalizika huku Yanga wakitoka kifua mbele kwa bao la kuongoza,lililotiwa kimiani na Hamis Kiiza Dakika ya 45 ya mchezo.na sasa kipindi cha pili kimeanza muda si mrefu na mtanange unaendelea.
 Said Bahanuz wa Yanga akimtoka Beki wa Azam,Aggrey Moris.
 Wachezaji wa Yanga wakishangilia bao la kuongoza.

2 comments:

  1. imetulia.yanga ni timu bwana ackwambie mtu eti.

    ReplyDelete
  2. HONGERENI SANA VIJANA WA YANGA KWA KUTWAA KOMBE LA KAGAME

    ReplyDelete