HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, July 22, 2012

BIOGRAPHY YA MZEE JOHN KITIME NJE YA MUZIKI

Naitwa John Kitime, nilianza kufurahia vichekesho mara baada ya kuzaliwa na kukuta watu wazima kila wakinichukua walijitahidi kunichekesha kwa kuanza kuonea lugha ambayo sijaijua mpaka leo, maana mara alikuja mmoja na kuanza 


bujibujibujibujibuji,jigijigjigjigjijij, grugrugrugru’ na maneno mengine ya ajabu nilijitahidi kuwavumilia nisiwacheulie maziwa lakini baadae nikagundua heri niwe nacheka wakianza vituko hivyo, mana baada ya hapo walikuwa wanajiona wanajua kuchekesha watoto wachanga.


Niliendelea kukua nikaanza shule nakukuta vituko vingi sana vya kuchekesha, kama vile watu kujikojolea darasani, hili bahati mbaya nililikuta linajirudia pia kuwakuta wakubwa wakijikojolea kwenye baa, ene way, nilimaliza shule na kujiunga na chuo na huko nilijifunza utalaamu wa kunywa pombe na baada ya hapo nilikutana na watu wengi wenye kujua kuchekesha, kucheka na hata wasiojua kuchekesha , wengine hawajui kucheka kabisa, au wanaweza kucheka mahala pasipo na kichekesho.


Katika kiota hiki ntaweeleza mengi yaliyonikuta katika maisha yangu haya yaliyojaa furaha sana NAMSHUKURU MUNGU.


Pia mimi ni mwanamuziki napiga gitaa naimba kwenye bendi, lakini huwa sichezi, sijui kucheza, hasa Chacha ndio kabisa halafu siku hizi kuna hii inaitwa Kwaito, wakati najitahidi kujifunza imeanza Kiduku, sijaishika sawasawa imekuja Kibajaji heee jamani si mngoje japo nijuwe staili moja ndio mbadili? 


Halafu huwa inanishangaza, mtu analipa kuingia muziki halafu anacheza kuliko sisi wanamuziki jamani, mnajua mngepewa majembe mlime badala ya kucheza mngesha maliza tatizo la njaa hapa nchini?


JFK


BOFYA HAPA KUONA LIBENEKE LAKE JIPYA

2 comments:

  1. hey there and thank you for your information – I’ve definitely picked up anything new from right here. I did however expertise some technical issues using this website, as I experienced to reload the web site a lot of times previous to I could get it to load correctly. I had been wondering if your web hosting is OK? Not that I am complaining, but sluggish loading instances times will very frequently affect your placement in google and could damage your high quality score if advertising and marketing with Adwords. Well I am adding this RSS to my email and can look out for a lot more of your respective exciting content. Ensure that you update this again very soon.. biography

    ReplyDelete

Post Bottom Ad